Je!, Bwana huokoa watu gani?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 37:39,40 Na wokovu wa wenye haki una BWANA; yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
Unapojikuta kwenye shida, kitu ambacho hakina budi kutokea mara kwa mara, je! Una ujasiri kiasi gani kwamba Bwana atakuonekania na kukuokoa? Kama ungepima ujasiri wako na kujipaita maksi kati ya sufuri na kumi, ungekuwa na maksi gani? Kwa nini umejitathmini hivyo?
Ni swali linalosumbua, sindiyo?, Mfano, mimi niko kwenye shida kubwa, halafu hata sijui imetokea wapi, halafu mambo yanazidi kuniharibikia, e! Ni lini Mungu ataingilia kati na kuniokoa na shida zangu? Hivi aataonekana kweli?
Jibu ni kwamba, inategemeana. Inategemeana hasa na namna mtu alivyo.
Zaburi 37:39,40 Na wokovu wa wenye haki una BWANA; yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
Hata kama wewe na mimi hatutaki kukubali, mara nyingi tunaingia kwenye shida kwasababu tumefanya makosa! Amina??
Na kama ndivyo ilivyo, ni rahisi kukata tamaa huku tukijua kwamba ni halali kupata matatizo, na nirahisi pia kufikiri kwamba Mungu hatajihusisha kabisa na matatizo hayo.
Kama baba mzuri, Mungu anaweza kuruhusu tuendelee kupitia matatizo hayo kwasababu ni sehemu ya fundisho. Lakini tukumbuke kwamba, Mungu anatupenda sana zaidi ya baba mwema wa kimwili awaye yote duniani!.
Na wokovu wa wenye haki una BWANA; yeye ni ngome yao wakati wa taabu. Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa; kwa kuwa wamemtumaini Yeye.
Usifikiri kwamba muda umeshapita wa kuanza kutenda mema, hapana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.