... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuinuliwa Katika Unyenyekevu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 2:7-9 Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina.

Listen to the radio broadcast of

Kuinuliwa Katika Unyenyekevu


Download audio file

Inapendeza kweli hasa pale watu wengine wanapokuthamini vile ulivyo. Ni jambo jema sana.  Lakini tunaishi katika ulimwengu ambao watu wamevuka mipaka kabisa kwa swala la kupongezana.

Kubadilishwa ili mtu afanane na Yesu zaidi si swala linaloweza kukamilika kwa siku moja.  Kwangu mimi haikutokea hivyo.  

Sasa, kwa kuwa tuko sambamba, tufanyeje sasa na nia ya kutaka kupendwa ambayo imo ndani ya kila mwanadamu, kufikiriwa vema, kupongezwa na kusifiwa jinsi tulivyo wazuri sana? 

Kwasababu unajua kuthaminiwa na wengine ni jambo tofauti kabisa na mtu kutamani kujulikana na kupongezwa au kupewa tuzo.  Ebu, tumtazame Yesu kwanza: 

Wafilipi 2:7-9  Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.  Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina. 

Maneno hayo yananielezea kwamba, kwa kujitoa kwa tendo la unyenyekevu, Yesu alistahili kuadhimishwa mno na kupata tuzo ya kipekee kuliko zote.  Sasa, kanuni hiyo ndiyo inayoweza kutenda kazi hata ndani ya watu wa kawaida kama mimi na wewe. 

Mtu akiendelea na safari akiwa pamoja na Yesu – hata kama siku zingine hapigi hatua vizuri – ndipo atagundua kwamba kadiri anavyojishusha, kadiri anavyoachana na nia ya kutambulika na kutafuta kupongezwa na watu wa ulimwengu, ndivyo atakavyozidi kufurahia baraka ya kuwekwa huru na mtego ule, asiwe tena na haja ya kushangaza watu na kujulikana na kutafuta ushindi daima. 

Pia, mtu akijinyenyekeza Mungu ana njia nyingi sana za kumbariki kuliko unavyoweza kufikiria, jinyenyekeze.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.