... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Sehemu Maradufu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Sehemu Maradufu 2 Wafalme 2:9 Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondoka kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.

Listen to the radio broadcast of

Sehemu Maradufu


Download audio file

Najiuliza, sijui kama umeshawahi kujisikia kama mimi, yaani unamtumikia Mungu kwa nguvu zako zote huku ukijaribu kutenda mema kwa ajili yake … lakini ni kama inakuwa ngumu sana. Ni kama Mungu hayupo, yaani ni kama unabeba mzigo peke wote peke yako.

Ni kweli, ninaelewa kwamba wasikilizaji wangu wengine wanaweza kufikiri labda mimi sina nia hata kidogo ya kumtumikia Mungu, kweli beni uko siriasi?!:  Sawa, Lakini hata hivyo, wengi wetu tunataka kutenda mema, si kweli?  Lakini kutenda mema wakati mwingine ni kazi ngumu. 

Kadiri ninavyozidi kuzeheka, ndivyo ninavyoachana na jitihada za kutumika kwa nguvu zangu. Kwa kuwa tunaye Mungu mwenye uweza wote, mwenye rasilimali zote akiwa na nia ya kutubariki pia, kwanini mtu atamani kutumika kwa nguvu zake mwenyewe? 

Zamani katika Agano la Kale kulikuwa na nabii mkubwa aitwaye Eliya aliyekuwa na mwanafunzi wake Elisha. muda wake kuondoka kwenda kwa Mungu ulipowadia … basi acha nikusomee: 

2 Wafalme 2:9  Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondoka kwako.  Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu. 

Kwa kuomba hivi, ni dhahiri kwamba Elisha hakutaka kutumika kwa nguvu zake. Na lile aliloomba ndilo alilopewa. Wakati Eliya anapelekwa juu, sehemu maradufu ya Roho wa Mungu ilimwangukia Elisha – na kumpa uwezo mkubwa na mamlaka kubwa.

Kujikumbusha:  Acha kutumika kwa nguvu zako mwenyewe.  Omba Mungu akupe sehemu maradufu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.