Kukabiliana na Dhoruba Peke Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 8:23-27 Akapanda chomboni, wanafuzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?
Hakuna hata mmoja wetu anayefurahia misukosuko ya maisha japo haina budi kutokea, sindiyo? Sasa mtu anapokuwa katikati ya dhoruba, mara nyingi huwa anajiona kama yuko peke yake.
Yamkini unamwamini Yesu. Pengine wewe ni mwanamume au mwanamke wa Biblia na unafahamu kwamba katikati ya misukosuko ya maisha, inatakiwa umtegemee Mungu. Sawa kabisa! Lakini tuwe wawazi ndugu. Dhoruba inapopiga kweli kweli huwa inaonekana kama Yesu amesinzia, huwa inafanya Yesu aonekane kama hana msaada kabisa , Au labda ni mimi tu naweza hivyo!?
Mathayo 8:23-27 Akapanda chomboni, wanafuzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?
Leo asubuhi nilipokuwa ninaandaa kipindi hiki kulikuwa na dhoruba kubwa sana huko nje. Ebu fikiria ingekuwaje kwa mabaharia walioko huko baharini katika hali kama hiyo!!, Binti mmoja alisema hivi … “Kuwa na Yesu chomboni haimaanishi kwamba hutakabiliana na misukosuko. Lakini inamaanisha kwamba hakuna dhoruba itakayoweza kuzamisha mtumbwi wako. Tembea kwa imani na kamwe hautatembea peke yako.”
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.