Makosa Wanawake Wanayofanya (1)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 31:10-12 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake.
Mimi naona kama kosa kubwa la akina mama wanalofanya katika ndoa zao ni hili: wanapoanza kupata uzao, wanaweka wanaume zao kwenye nafasi ya tatu, nne au ya tano katika ngazi ya familia. Ni kosa kubwa sana.
Sasa kama unafikiri kwamba ninawavizia akina mama, ujue kwamba siku hizi mbili zilizopita, tulisimulia makosa makubwa akina baba wanayoyafanya. Sina ubaguzi bali nataka kutamka hekima ya Mungu kwa ajili kukarabati na kuimarisha familia.
Kweli, uhusiano kati ya mama mzazi na watoto wake ni ya kipekee. Si aliwabeba mwilini mwake na akawazaa – yaani ni mwambata ambao sisi wanaume hatuwezi kuelewa hata kidogo.
Lakini bila mume, bila baba mzazi, watoto wasingalikuwepo. Pia, bila mahusiano mazuri kati ya mke na mume, nakwambia, watoto watatoka relini na kuharibika; familia itasambalatika. Kwa hiyo kama wewe ni mwanamke, nisikilize:
Mithali 31:10-12 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake.
Kumbe! kiwango ni cha juu sana – mke mwema aliyekamilika, mke ambaye mume wake humwamini, amtendea mema siku zote wala si mabaya .
Ninyi wake, hata kama waume wenu wanataka kuwalinda na kukidhi mahitaji yenu, wao pia wanahitaji muwategemeze. Kama unataka ndoa yako iimarike, acha nikuonyesha la kufanya. Usimshushe hadhi mume wako, asiwe tena kipaumbele machoni pako, wala usimsumbue hata siku moja.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.