... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Moyo wako umefunguliwa … au umefungwa?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ufunuo 3:19,20 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Listen to the radio broadcast of

Moyo wako umefunguliwa … au umefungwa?


Download audio file

Kinachochukiza sana kwa kuwa Mkristo ni hatua ya kutubu; kuachana na yale ambayo tunafahamu kuwa ni mabaya.  Ndio maana watu wengi wanasita kumjia Yesu.

Kinachomwia vigumu mtu kutubu (niwie radhi kwa neno hili nitakalotumia) ni kutokukubali kwamba amekosea, lakini kiburi chake kinaleta kikwazo.  Pia, mtu atakuwa ametawaliwa na dhambi yake anayopendelea.  

Lakini kwasababu Mungu anatupenda, hawezi kuruhusu tuendelee kujidanganya.  Yesu hawezi kabisa, pia aliongea hivi … 

Ufunuo 3:19,20  Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.  Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 

Yesu anafahamu kwamba tukiendelea na dhambi, itatupelekea kwenye mauti ya milele, na kwa kuwa anatupenda, ujue kabisa kwamba hawezi kuachilia, bali atasababisha mambo yafikie muda wa kufanya maamuzi; yaani atatukemea na kuturudi hadi pale itakapotulazimu kuchagua kitu kimoja au kingine. 

Tunaweza kuwa na bidii na kutubu au tunaweza kumpinga, hata kama kufanya hivyo haieleweki.  Ni kweli, ni vigumu sana kutubu, lakini tunaposikia sauti yake, je!  Tutamfungia mlango mioyoni mwetu? 

Wewe vipi?  Je!  Umemfungulia mlango au bado umefungwa?  Je!  Utatubu au utakosa kushirikiana naye? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy