... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usimwonee Haya Yesu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 12:8,9 Nami nawambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Usimwonee Haya Yesu


Download audio file

Nadhani umeshaona kwamba inazidi kuwa vigumu kukiri hadharani kama unamwamini Yesu.  Lakini huyu Yesu ndiye ametuagiza tumtii, ndiye asemaye kwamba haki inabaki kuwa haki na uovu unabaki kuwa uovu.

Ni kweli kabisa.  Imeanza kuwa vigumu.  Sehemu ya timu yetu ya hudumu hii wanaishi kwenye nchi ambazo makanisa yanachomwa moto na wachungaji wanafungwa, wengine wanatendewa vibaya. 

Katika sehemu zingine za ulimwengu, kama vile hapa ninapoishi, tunabanwa mno, wanataka tuachane na msimamo wetu wakidai kwamba umepitwa na wakati, kwamba mtu hawezi kusema hiki ni haki na kile ni kibaya, wanapinga habari za Yesu. Wanatumia mapambano ya fikra, wakijaribu kufuta mawazo mengine kwa kusababisha jamii iyaonee karaha mambo ya Kristo. 

Sasa mtu atafanyaje?  Si swali la ki-nadharia tu.  Ni swali ambalo kila mmoja wetu ni lazima alijibu kwenye dunia hii inayozidi kuchukia Ukristo.  Sasa tufanyeje? 

Tunaweza kujisalimisha na kunyamaza kana kwamba tunakubaliana nao, au tunaweza kwa upole na upendo, kuwa na msimamo wa kumtetea Kristo na kuwa tayari kulipa gharama?.  Sikiliza alivyosema Yesu: 

Luka 12:8,9  Nami nawambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu. 

Kusimama kidete na kumtetea Kristo itakugharimu – labda kidogo, labda sana, inategemeana.  Lakini jipe moyo.  Usimwonee haya Yesu na yeye hatakuonea haya. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.