Rafiki Kama Hawa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 5:17-20 Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.
Ninalo swali kwako leo: Je! Unao rafiki wa namna gani? Rafiki wema, rafiki waaminifu, rafiki wa hivi-hivi au rafiki wasio rafiki kweli? Unao rafiki wa namna gani?
Haijalishi una akili gani au kama wewe ni mwerevu sana au mwenye nguvu, hakuna awezaye kuishi peke yake. Kila mtu anahitaji kutiwa moyo na kuonywa pia, kuwa na uhuru na nidhamu pia, kutegemezwa na kutegemeza wengine pia. Hii ilikuwa mpango wake Mungu kwetu. Sasa jinsi tunavyowachagua rafiki zetu, kwa kweli inaleta matokeo katika aina ya maisha tutakavyoishi.
Kuna rafiki ambao tunasoma habari zao ndani ya Biblia na kila zinatushangaa mno.
Luka 5:17-20 Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya. Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Je! Unao rafiki ambao wangepenya ndani ya umati wa watu wakikubeba kwenye kitanda ili uweze kumwona Yesu? Rafiki ambao wangepanda dari na kuibomoa ili wakushushe miguuni pa Yesu? Watu ambao wangethubutu hivyo kwa ajili yako? Kama huna … basi watafute!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.