... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Siku Ile Inakuja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Malaki 4:1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.

Listen to the radio broadcast of

Siku Ile Inakuja


Download audio file

Hukumu ya Mungu iwakayo moto si jambo ambalo watu wanataka kuliamini.  Ni dhana isiyoeleweka pale mtu anapofikiri habari za Mungu wa upendo … Tena hakuna mtu anayependa kutendewa hukumu kama hiyo!

Miaka kadha iliyopita, kulikuwa na mwanariadha maarufu aliyeishi karibu na nyumbani kwetu, Sasa yeye alitaja mistari ya Biblia kwenye mtandao inayosema habari za hukumu ya Mungu; na ukweli wa uwepo wa Jehanamu, sehemu ya mateso yanayoendelea milele. 

Alizomewa kabisa na kutukanwa vibaya na watu ambao hawaamini kwamba kuna Mungu, hadi alipoteza ajira yake katika mchezo huo.  Swali linakuja mara moja.  Je!  Kwanini kundi lile la wakana Mungu walikwazwa mno na mada ile?  Si wanasema wao wenyewe kwamba hakuna Mbingu wala Jehanamu? 

Lakini kwenye kiini cha mioyo yetu sisi sote tunajua kwamba lazima tutoe hesabu mbele za Mungu siku moja, tupende, tusipende. 

Malaki 4:1  Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. 

Maneno hayo yanaleta picha inayotisha, ni maneno mazito yanayohusu namna mtu atajieleza kwa kutoa mahesabu. Mtu kuitwa ili atoe mahesabu si jambo baya bali ni jambo linalofaa. Kila mtu atawajibika kutoa maelezo ya matendo yake. Pia, lazima matokeo yawepo kutokana na mwenendo mbaya. 

Kwahiyo kuna maswali yatupasa kuyajibu kama sisi tunavyomwamini Yesu.  Je!  Nimeanza kuwa mwenye kiburi?  Je!  Nimeanza kutenda uovu?  Ni kweli, tunajua kwamba mtu anayemwamini Yesu anaokolewa na hukumu kwa imani ndani yake. 

Lakini mtu akimpa Mungu kisogo, akijaa kiburi, akichagua kufuata njia ya uovu … aangalie!  Siku ile inakuja.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.