... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usikawie, Kwa Sababu …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Petro 3:10-12 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?

Listen to the radio broadcast of

Usikawie, Kwa Sababu …

Download audio file

Siku moja vitu vyote vitafikia ukomo.  Mbingu na nchi zitapita.  Je!  Tukio hilo kubwa unalitazamia kwa shauku?

Jibu lako linategemeana na mahusiano uliyo nayo na Mungu.  Kwa sababu sisi sote tutakuwepo siku ile, tukielekea njia moja au nyingine.

2 Petro 3:10-12  Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.  Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?

Jana tuliongea habari za uvumilivu wa Mungu, huruma zake na neema yake, sifa tunazoweza kutegemea tunapojikwaa na kuanguka, zikitusaidia kumrudia kila wakati na kumuomba msamaha wake.  Tusikose kukumbuka jambo hilo wala tusilitie mashaka kwasababu huruma zake zenye uvumilivu pamoja na neema yake vitatuelekeza taratibu-taratibu tufikie toba.

Lakini haitupasi kusahau kwamba mwisho utafika kama mwivi wa usiku. Halafu mwisho ukifika, utakuwa mwisho wa safari yetu, wewe na mimi.  Nafasi ya kutubu itakuwa imeshapita.  Sasa leo, kuna ujumbe gani katika neno hilo kwa ajili yetu?

Imetupasa sisi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa?… kwa kuwa mwisho unaweza kuja haraka kuliko unavyofikiria.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy