... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuwa na Subira Wakatiwa Mateso

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo5:11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.

Listen to the radio broadcast of

Kuwa na Subira Wakatiwa Mateso


Download audio file

Ni matatizo gani ambayo unapambana nayo muda huu?  Ni kipi kinachokutafuna na kupunguza hamu ya kuendelea kuishi?  Je!  Utwambie, unakabilianaje na matatizo yako?

Kuna watu wengine wanaonekana, ukiwatazama kwa mbali, kwamba wana maisha bora.  Lakini bila sisi wengine kujua, wanakosa amani, wanateswa na hali ya kutoridhika kiasi cha kushindwa kuielezea. 

Kuna wengine pia ambao kwa mtazamo wetu sisi wengine, nikama maisha yao yamevurugika kabisa.  Lakini hatahivi, wanaonekana kwamba wanaamani.  Wanatabasamu sana kuliko inavyostahili.  Kuna furaha ya kina moyoni mwao ambayo haieleweki kibinadamu.  Inawezekanaje?

Yakobo5:11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri.  Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana yakwamba Bwana nimwingi wa rehema, mwenye huruma.

Kukubali kuvumilia katika mateso ni kanuni isiyorahisi lakini Yakobo akiwaandikia Wakristo hawa walioteswa na kutawanyika kote duniani ,anatoa ushahidi uliowazi akiwakumbusha juu ya dhiki kubwa iliyompata Ayubu katika Agano la Kale.  Matatizo makubwa mno!

Hatimaye Mungu alifanyeje?  Bwana alimsaidia sana kama unavyojua ikiwa ulishasoma habari hii.  Ni ushahidi tosha kwamba Bwana Mungu wetu amejaa huruma na fadhili.

Je!  Mtu anawezaje kuvumilia katika mateso?  Kwa kupokea moja kwa moja kweli hii kwamba Mungu ni mwenye huruma na fadhili kabisa kabisa.  Sasa, kishakuelewa hayo kunakuja furaha, na uvumilivu na amani …kwa kifupi, baraka zake.  Uwe nasubira.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.