Kumtafuta Yeye Bwana
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 86;5,6 Kwa maana wewe, Bwana, u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; uisikilize sauti ya dua zangu.
Mateso yakikujia tena, je! Ni kwa kiwango gani unachotaka kutafuta uso wa Mungu? Jibu la watu wengi linawezakuwa, sio sana. Kwa hiyo wengi wanakaa tu na kuingiwa na wasiwasi kana kwamba itasaidia.
Jana tuliongelea habari zinazohusu ukweli wenye nguvu wa ujio wa Yesu duniani, ujio unaoweka watu huru na kubadilisha maisha yao akiwatafuta na kuokoa waliopotea. Watu wabaya sana kama Zakayo, mtoza ushuru ambaye Yesu alitaja habari zake akisema:
Na huyu pia ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.
Ni habari njema kabisa … kusikia kwamba anatafuta wenye dhambi kama wewe na mimi. Hatuna sababu ya kumkimbia wala kuwa na hofu na aibu katika mateso yetu. Bali inatubidi tukimbilie kwake kama vile alivyoandika Mfalme Daudi wa Israeli, miaka elfu moja kabla Yesu hajazaliwa:
Zaburi 86;5,6 Kwa maana wewe, Bwana, u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili, kwa watu wote wakuitao. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; uisikilize sauti ya dua zangu.
Wakati wa mateso – labda kwa sababu alizoea kupitia mateso mengi – mara moja Daudi alimgeukia Mungu na kumlilia na kumsihi hivi – Uisikilize sauti ya dua zangu.
Unajua, alikuwa na silka sahihi.kwa sababu Yeye ni Mungu wa neema na rehema, Mungu wa upendo na msamaha. Ndivyo alivyo. Ndio maana alimtuma Yesu kuja kukutafuta. Ndio maana ana shauku kusikia unamlilia.
Umtafute Yeye,Anapatikana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.