... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupata Raha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yeremia 31:25 Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni.

Listen to the radio broadcast of

Kupata Raha


Download audio file

Ni mara chache sana kusikia watu wanaokuwa na nafasi kama ya kwangu kukiri kwamba wamechoka. Si unajua mimi ni muhubiri, lazima niwe na majibu yote.  Lakini si kweli, tena sisi wahubiri tunaweza kuchoka, tena kuchoka mno.

Ni kweli, kuna wakati uchovu na udhaifu unafika nyumbani kwangu. Hata kama nina afya njema, nikifanya mazoezi, hata kama ninakula kama inavyotakiwa, hata kama ninaweka kipaumbele muda wa kumpumzika na kukaa na familia, bado kuna wakati ninamezwa na mambo mazito ya kunichosha. 

Kuna sababu nakwambia haya. Ninataka uwekwe huru kwa kutambua kwamba si wewe tu unachoka sana. Uchovu unakuja kwa njia mbalimbali: Kwanza, mwili kuchoka, hii ni dhahiri, lakini kuna kuchoka kihisia na kiroho pia.  Kuna wakati ni kama dhoruba mtu akichoshwa kimwili, kihisia na kiroho yote kwa pamoja!

Kwahiyo, mtu atajisikia kwamba amelegea sana, akichoka kiasi hawezi tena kupambana katika ulimwengu huu hata kujisikia kwamba yeye ni mnafiki.  Mimi ninajiita Mkristo, mtu anayemwamini Mungu.  Kwa nini mambo hayaendi?  Nimekosea wapi? 

Fungua Biblia yako, soma habari yoyote ile – kuanzia Adamu na Hawa, kupitia akina Musa na Ibrahimu, na Yusufu na Daudi … hadi Mtume Paulo katika Agano Jipya na hata Yesu mwenyewe – na utagundua kwamba uchovu uliwapata kila mmoja.  Acha niseme tena.  Asilimia mia ya mashujaa wale ndani ya Biblia waliwahi kushikwa na uchovu mkubwa. Kwahiyo, mtu afanye nini?  Jibu liko wapi?  Tegemea Mungu: 

Yeremia 31:25  Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni. 

Charles Spurgeon aliwahi kusema hivi:  “Jitupe kwenye uaminifu wake Mungu kama vile unajitupa kitandani wakati unachoka, ukimletea yeye fadhaa zako zote ili akupumzishe.” Wakati mambo hayaendi kabisa, jitupe juu ya Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.