Unifundishe
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Dalili kubwa ya unyenyekevu mtu anaweza kuwa nayo kuliko zote ni kuwa na moyo unaofundishika. Kwa kweli, bila moyo kama huo, mtu hawezi kuishi kwa unyenyekevu.
Unyenyekevu unapendeza sana, hususani, ukionekana ndani ya watu wakubwa wenye vipaji. Wewe na mimi tunapendezwa tukikutana na unyenyekevu ndani ya watu wengine kwa sababu hua unatanguliza ubinadamu wao; wanakuwa sawa na sisi, wakitukaribia na kutujali kwa jinsi wenye kiburi na jeuri wasingeweza kufanya.
Sasa, je! Ndivyo watu wengine wanavyokuangalia? Uwe mkweli. Wewe una ujuzi wako na vipaji katika maisha – mambo ambayo unaweza kuyafanya vizuri kuliko awaye yote unayemfahamu. Sasa uwezo wako huu, unauleta mezani kwa unyenyekevu, au wewe ni mtu anayetaka kukandamiza wengine kwa kiburi chako?
Mfalme Daudi alikuwa na mamlaka mkubwa kuliko wote katika Israeli zamani. Si kwamba alikuwa na madaraka juu ya maisha ya kila mwananchi tu, lakini pia alikuwa shujaa wa vita, akiongoza Israeli kupitia vita vingi. Alikuwa mwenye vipaji, mwenye nguvu, lakini aliomba hivi:
Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Hayo yanaonyesha moyo unaofundishika. Moyo wenye shauku wa kutenda njia za Mungu, si kuzijua kichwani tu. Halafu kwa sababu alipitia mambo mengi magumu katika maisha yake, Daudi alikuwa na uhakika kwamba akisimama katika mapenzi ya Mungu, Mungu angemwongoza kwenye nchi sawa.
Sasa tuapaze sauti tumwambie Mungu … Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.