... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiruhusu Imani Yako Ififie

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 12:1 Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.

Listen to the radio broadcast of

Usiruhusu Imani Yako Ififie


Download audio file

Je!,Umewahi kujikuta kwamba imani yako inaanza kupungua?, Mwanzoni, yaani zamani, ulikuwa unawaka moto kabisa kwa ajili ya Bwana.  Lakini moto ule umefifia, umebaki kama kaa tu na wakati mwingine ni kama majivu matupu.

Siku zilizopita, mwanamke fulani anayepata ujumbe wetu mfupi wa kila siku, aliomba msaada kwa ajili ya imani yake iliyokuwa inafifia. Alitaka iwe imara kila wakati. aliomba, asaidiwe na afundishwe namna ya kuimarisha imani yake.  Kwa hiyo tunataka kuanza kumjibu kwa siku kadhaa na inaweza kusaidia hata imani yako iimarike pia! 

Kweli, Mungu anajishughulisha na swala la kukuza imani yako ndani yake, kabisa! Lakini kwa kufanya hivyo, anahitaji ushirikiano wako (na wangu pia).  Kwa sababu kuna mambo tunayoyafanya, wewe na mimi yanayosababisha imani zetu zififie. 

Waebrania 12:1  Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu.   

Imani kubwa ya wale waliotutangulia na wale wanaotuzunguka, inatakiwa ihimize imani yetu pia. Safi kabisa, ndivyo inavyopaswa kuwa.  Lakini kuna sharti moja: 

Tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi. 

Je! Unabeba mzigo gani unaokukwamisha?, Je! Ni dhambi gani unayoushikilia inayosababisha uanguke? Kuachana na mambo yanayopinga imani yako, ni hatua kubwa yenye maana katika swala la kuimarisha imani yako.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.