... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Heri Mtu Astahimiliye …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 1:12 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Listen to the radio broadcast of

Heri Mtu Astahimiliye …


Download audio file

Majaribu yana vishawishi vingi,  na huwa yanamvuta mtu kwa nguvu.  Ndiyo asili ya jaribu lolote na ndio sababu huwa zinaleta madhara makubwa endapo mtu amekubali kushawishika. Pia, mara nyingi majaribu huwa yanatushambulia kwa ghafla, bila hata yakutazamia.

Nadhani sisi sote tumeshapitia hayo. Mambo yanaenda shwari kama kawaida, halafu ghafla, jaribu dogo linakuja likiwa limejaa vivutio vitamu halafu ghafla linavamia kwa nguvu.  John Wesley alisema hivi:

“Kama vile kimbunga kinavyoweza kuipiga, ndivyo hatari ya Shetani invyoingia kwa kupitia matukio madogo-madogo ambayo yanaonekana kuwa hayana maana sana, lakini kumbe yanaweza kumfungulia moyo pole pole na hatimaye kuleta madhara makubwa sana.”

Ni maneno ya kweli kabisa!  Na ndio maana kuruhusu maafikiano madogo-madogo na dhambi bila kuwa makini ni hatari sana. 

Lakini majaribu huwa yanakuja ghafla na kutoweka ghafla pia.  Dakika moja hakuna jaribu, dakika nyingine linakushambulia tena– halafu ghafla tena linatoweka.  Cha muhimu ni maamuzi yetu pale tunaposhambuliwa. 

Yakobo 1:12  Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 

Wakati wa mashambulizi tunaweza kuamua kushindwa au kustahimili.  Majaribu yanapima imani yetu kama ni ya kweli. Yanapima uimara wa tabia yetu ndani ya Kristo pia.  Halafu kila wakati mtu anapostahimili majaribu na kushinda ndivyo anavyozidi kufanana na Yesu. 

Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.