... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ndiyo maana Huwezi Kumbadilisha Mwingine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 2:24-26 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.

Listen to the radio broadcast of

Ndiyo maana Huwezi Kumbadilisha Mwingine

Download audio file

Kinachoweza kukatisha tamaa katika mahusiano ni kwamba, kuna watu wengine ni wazito sana. Umeshaona ukaidi wao, sindiyo?  Yaani Hawaweza kubadilika kabisa.

Nadhani unaelewa tunachokiongelea. Sisi sote tumeshuhudia hayo, Unaweza kuona wazi kabisa mtu anakosea; na anakoelekea ni kubaya panaweza kumletea madhara makubwa lakini asikubali ushauri wako wala hata asitake kukusikiliza kabisa. Ni kwanini? 

Nilisoma maneno umakini sana yanayojibu swali letu lakini sijui aliyeyaandika ni nani:  maneno hayo yanasema hivi, Ebu fikiria na kutafakari namna ilivyo ngumu wewe kubadilika  ndipo utakapoelewa kwamba itakuwia vigumu mno kuwabadilisha watu wengine. 

Ni kweli kabisa, sindiyo?!  Sasa, tunamwitikiaje mtu mkaidi kwa njia inayompasa mcha Mungu? 

2 Timotheo 2:24-26  Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake. 

Mwitikio wa ki-Mungu ni kuwa mwanana, mvumilivu, na mpole tukijaribu kuelemisha … kufanya hivyo kunampa Mungu nafasi ya kutenda kazi.  Tena tunajua yeye tu ndiye awezaye kumbadilisha mtu.  Mungu peke yake ndiye awezaye kumweka mtu huru mbali na mtego wa Ibilisi.  Tumia fadhili, uvumilivu, na upole.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.