Timiza Ahadi Zako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 5:37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

Wengi wetu tunapenda kuamini watu wengine. Je! ni kila mtu anaaminika? tunaweza kumtegemea?
husiano wa mmoja na mwingine hua inatokea mara kwa mara katika ulimwengu wote kwa kutumia maneno, kwa maandishi, hata mwili mwenyewe wa mwanadamu unaweza kuashiria hisia zake za ndani. Pia watu wanao utamaduni wao unaowawezesha kuwasiliana kwa jinsi yao.
Kwa hiyo, je! Wewe ni mtu unayetimiza ahadi yako? Je! Wewe ni mtu ambaye ahadi zako zinaaminika?
Yesu ni mtaalamu wa kurahisisha mambo kwa maneno machache yenye maana
Mathayo 5:37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Ni rahisi, si kweli? Maneno yako yawe Ndiyo, “ndiyo”; Siyo, “siyo”. Ina maana, inatakiwa uwe mwanamume au mwanamke anayeaminika. Usiweke makona mengi kwenye maneno yako. Toa wazi nia yako na weka bayana ahadi yako.
Ni kweli, kuna tofauti ndogo katika maana ya maneno kufuatana na tamaduni mbali mbali. Mfano, mtu kutoa kusudi lake kwenye utamaduni wa Asiya ni tofauti sana na jinsi mtu wa Magharibi angefanya. Lakini mwisho wa siku, ni rahisi tu.
Maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.