... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Kristo Anakuita

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Peter 2:21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Kristo Anakuita


Download audio file

 Je!  Umewahi kuhisi kwamba Mungu amekuitia kazi fulani uifanye kwa ajili yake?  Nadhani umeifahamu sauti ile mwororo, Hua inasumbua kidogo kwa sababu unafahamu kwamba utaumia.

Baadhi wanaweza kuwa na wito na kuwa mishonari kwa nchi ya mbali.  Wito wa Kristo dhidi ya maisha yetu unakuja kwa njia tofauti-tofauti lakini kila wito lazima ufanane na mwingine.

Ninamfahamu mwanamke mmoja aliyeendelea kuwa mwaminfu kwa mume wake hata kama yeye alifululiza tabia ya uzinzi.  Namfahamu mwanamume ambaye amekuwa na mke kwa miaka mingi hataki kukaribiana naye kwa tendo la ndoa lakini bado amebaki mwaminifu kwake.  Ninamfahamu mishonari ambaye aliitikia wito wa Kristo kwenda ng’ambo ya bahari lakini alifanya wito kwa miaka michache akihama-hama bila kujua kinachoendelea. 

Watu wote hawa wanafana kwa kitu hiki kimoja.  Waliteswa.  Kwa nini iko hivi?  kama vile J.C. Ryle, Askofu Mkubwa wa kwanza wa Liverpool mnamo mwaka wa 1880 alivyosema: 

Itamgharimu mtu kuwa Mkristo wa kweli.  Tusisahau kweli hii.  Kuwa Mkristo wa jina tu, mtu wa kuingia na kutoka tu ni rahisi sana, si vigumu.  Lakini kusikia sauti ya Kristo, kufuata Kristo, kumwamini Kristo, kumkiri Kristo, itakugharimu na itabidi ujikane kabisa. 

Na kama vile Mtume Petro alivyoeleza: 

1 Peter 2:21  Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 

Kumbuka hili, itakugharimu kuwa Mkristo wa kweli.  Lakini ndio ulioitwa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.