... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kinachofuata

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 28:19,20 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana , na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Listen to the radio broadcast of

Kinachofuata


Download audio file

Labda wewe ni mmoja wa wale watu ambao wamethubutu kumwamini Yesu – Mwana wa Mungu aliyekufa kwa ajili ya dhambi zako, akafufuka kutoka wafu ili akupe maisha mapya, Safi kabisa!  Lakini kinachofuata ni kipi?

Nilipogeuka na kuwa Mkristo nikiwa na umri wa miaka 36, Siku moja nilitaka kutoka nje kwakasi ili ni ubadilishe ulimwengu. kama vile Ignatius wa Loyola alivyosema, “Atakayeanza kurekebisha ulimwengu huu, lazima aanze kujirekebisha mwenyewe, la sivyo atahangaika bure.” 

Kwa hiyo “kinachofuata” ni swala la mahusiano yetu na Yesu, katika fikra zetu, maneno na matendo pia.  Sikiliza alivyoagiza Yesu kabla ya kupaa mbinguni, akitoa husia kwa wanafunzi wake. 

Mathayo 28:19,20  Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana , na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. 

Ni kweli, Yesu ametuita tuwe wanafunzi wake na kuenenda, huku tukitumia vipawa na vipaji alivyotukirimia kwavyo, kwa ajili ya kurekebisha ulimwengu, tukiwafanya watu wengine kuwa wanafunzi.  

Kwa hiyo, kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo ni kufuata yote, Kwanza kabisa ni kukua katika kumtii yeye na kushirikisha wa-ulimwengu habari ya upendo wake. Hicho ndicho kinachotakiwa kuwa na  imani ndani ya Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.