... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usipange Kutenda Maovu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 14:17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.

Listen to the radio broadcast of

Usipange Kutenda Maovu


Download audio file

Mtu akiishi kwenye nchi kama hii yetu  ambayo imejaa wanyama wenye sumu kama – buibui na nyoka ni hatari sana, nakumbuka niliwahi kushambuliwa na kangaroo nilipokuwa mtoto, heee, ni balaa, yaani kule kwetu ukikutana na nyoka porini hasa kwenye majani marefu ni hatari, inatisha.

Yaani kumfananisha na nyoka mtu anayekuvizia kwenye maisha kwa lengo la kukuumiza ni sahihi kabisa. 

Mithali 14:17  Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. 

Jana tulizungumzia kuhusu uovu unaotokea ghafla – yaani mtu aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga, lakini hebu tuchunguze aina ya pili ya uovu. 

Mtu mwenye hila mbaya huzirwa.  

Hapo tumepata ainisho la  nyoka mviziaji kwenye majani,  mtu ana hasira halafu anapanga kwa hila zake kujilipiza kisasi,  Sikiliza, ukiona mawazo ya kulipiza kisasi yanazungukazunguka kichwani mwako na kutia sumu moyoni mwako, ujue unavutwa kwenda kinyume na kusudi la Mungu.

Je!  Hayo ndiyo kusudi la Mungu kwetu?  La!  Hasha!  Wakati mtu anapanga maovu kwa chini chini, akifikiri hakuna anayemwona, tunajua hakika kwamba Mungu anaona tena hafurahi. 

Hakuna apendaye mtu anayepanga uovu kwa hila – watu hawampendi na Mungu hampendi pia.  Usiwe kama ule nyoka anayejificha ndani ya majani.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.